chuo cha ufundi JITA

Kuhusu chuo cha ufundi JITA.

Chuo cha ufundi JITA kilianzishwa mnamo tarehe 11.4.2016 na kimesajiliwa na NACTVET kwa namba REG/NACTVET/VTC/0845 kutoa mafunzo ya ufundi kwa kozi za muda mrefu katika fani za;

  • Ususi na urembo (miaka miwili)
  • Ushonaji wa nguo (miaka miwili)

Na pia chuo kinatoa mafunzo kwa kozi za muda mfupi katika fani za;

  • Ususi na urembo (miezi 3)
  • Ushonaji wa nguo na kudizaini (miezi 6)
  • Upambaji wa kumbi (miezi 2)
  • Uokaji wa keki (mwezi 1)
  • Ufumaji wa masweta kwa mashine (miezi 2)
  • Kudarizi (miezi 2)
  • Utumiaji kompyuta (miezi 3)

Chuo cha JITA kinapatikana katika kata ya Mkundi, manispaa ya Morogoro km 10 kutoka stendi ya Msamvu kuelekea barabara ya Dodoma.

Wanafunzi

Kozi

Waalimu

KWANINI UCHAGUE CHUO CHA UFUNDI JITA?

  • Mazingira mazuri na tulivu ya kujifunzia
  • Darasani ni vitendo zaidi
  • Elimu za ujasiriamali kwa wanafunzi

MAONO YA JITA

Kuwa chuo bora cha ufundi Tanzania chenye kumjenga mtu kitaaluma, kiuchumi, kimaadili na kutokomeza umasikini katika jamii.

DHAMIRA YA JITA

Kuhamasisha, kuelimisha na kulea vijana katika misingi ya kimaendeleo kuhakikisha tunajenga taifa Imara.